Na Ester Macha,Mbeya.
Wamiliki wa makampuni ya ununuzi wa zao la pareto Mkoani Mbeya wametakiwa kufuata taratibu zilizowekwa katika ununuzi wa zao hilo ili kuwanufaisha wakulima badala ya kujinufainisha wamiliki pekee.
Mtakwimu wa bodi ya pareto Nyanda za juu kusini ,Tumaini Ngojile amesema ni vema makampuni yanayojishughulisha na ununuzi wa pareto kufuata taratibu zote zilizowekwa ili kuweza kupata mzazao bora kwa faida ya kulima ambaye kwa kiasi kikubwa ndiye anayeumia.
Ametaja taratibu hizo kuwa ni mnununuzi kuhakikishe ana leseni ya kazi, lazima anunue pareto inayoletwa kituoni na siyo kwenda majumbani kununua.
Aidha amesema wanunuzi wanatakiwa kutekeleza makubaliano yao kwa kuweka vibao vya majina ya makampuni na bei rasmi za ununuzi kwa siku husika ya soko.
Hata hivyo Ngojile amehimiza mizani zinazotumika zikaguliwe kabla ya kwenda kufanyia kazi ili kuepuka udanganyifu unaweza kufanywa na wanunuzi,alipiga maarufuku kununua pareto mbichi kwani inalenga kuzooretesha ubora wa zao hilo.
Aidha ametoa wito kwa wakulima na makampuni, wakulima wasikubali kuuza pareto kwa walanguzi kwani lengo lao siyo la kibiashara na badala yake wanalenga kuzoretesha zao hilo na kwamba makampuni yatakayobainika yanalangua na kununua pareto majumbani sheria kali zinachukuliwa.
No comments:
Post a Comment