Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, July 3, 2012

SERIKALI YAOMBA MSAADA WA MADAKTARI WA UPASUAJI - HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.



Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya umeiomba serikali msaada wa kupatiwa madaktari wa upasuaji kutokana na uchache wa madaktari uliopo hospitalini hapo.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dokta Eliuter Samky amesema hayo jana wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kuangalia hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa hospitalini hapo.

Dk.Samky amesema kuwa baada ya kufukuzwa kwa madaktari 72 huduma inayotolewa hospitalini hapo haikidhi matakwa kwa kuwa vitengo kadhaa vimeathirika sana.

Amevitaja vitengo vilivyoathirika kuwa ni kitengo cha upasuaji ambapo kuna madaktari wane, Madaktari bingwa  wanne akiwemo na yeye wakati kitengo cha macho nakuna Daktari kabisa.

 “Kwa kweli hali ya utoaji huduma imekuwa ngumu sana kwani tuna madaktari 39 tu hospitali nzima na katika hospitali ya wazazi wa Meta ni madaktari wawili tu wamebaki kwa kweli tunahitaji nguvu ya madaktari wengine kuja kutusaidia”.

Akijibu maombi hayo Kandoro amesema kuwa wanafanya utararitu wa kupata madaktari wa upasuaji kutoka katika hospitali za Wilaya za Kyela,Mbozi na Rungwe ili kuwapeleka Rufaa kusaidia kukidhi mahitaji ya wagonjwa.

No comments: