MWANDISHI MKUU WA MBEYA YETU JOSEPH MWAISANGO AKIWA KATIKA PILIKAPILIKA ZA KUPATA PICHA NZURI KATIKA UZINDUZI WA MRADI HUO WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA
Rais Kikweta amezindua mradi mkubwa wa maji uliokamilika kujengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 79.
Akizindua mradi huo, Rais Kikwete aliiagiza Wizara ya Maji kuanza kutafuta vyanzo vipya vya maji kwa ajili ya matumizi ya wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake vitakavyoanza kutumika ifikapo mwaka 2017.
Alisema kuwa mradi huo kwa sasa unao uwezo wa kuzalisha maji mengi kuliko uwezo wa matumizi ya wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake.
Alisema mradi huo unao uwezo wa kuzalisha maji lita za ujazo milioni 51 kwa siku wakati majitaji ya maji kwa wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake kwa sasa ni meta za ujazo milini 38 pekee.
Hata hivyo alisema kuwa kwa maehesabu ya kitaalam kuhusiana na ongezeko la watu katika Jiji la Mbeya, maji hayo yatakidhi mahitaji hadi mwaka 2017 na kuwa baada ya hapo vyanzo vingine vya mahitaji vitahitajika ili kutosheleza mahitaji ya wakati huo.
“Ifikapo mwaka 2017 tutahitaji vyanzo vingine vya maji, sasa sio vema wakati huo ukifika ndipo tuanze kuvitafuta, naiagiza Wizara ya Maji kuanza sasa kutafuta vyanzo hivyo ili muda huo ukifika tuanze kuvitumia,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema kuwa mradi huo umejengwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania iliyotoa Bilioni 29, Umoja wa Ulaya ulitoa Bilini 39 na Ujerumani iliyogharimia shilingi bilioni 13.
Awali akimkaribisha Rais Kikwete, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa mradi wa maji Mbeya kwa sasa ndio mkubwa kuliko yote nchini ambao umejengwa na kukamilika tayari kwa matumizi ya wananchi.
Alisema kuwa Umoja wa Ulaya na Ujerumani pia zimeisaidia Tanzania kujenga miradi ya maji katika mikoa ya Mwanza na , Iringa.
Alisema katika hatua ya pili ya ujenzi wa miradi ya maji nchini sasa itaanza kutekelezwa katika miji ya Bukoba, Mtwara, Lindi, Babati na Musoma.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni ukombozi kwa wakazi wa Jiji la Mbeya na Vitongoji vyake, ambapo sasa kila mwananchi anao uwezo wa kupata maji safi na salama.
Aliwataka wakazi wa Jiji la Mbeya kulinda na kutunza vyanzo na miundombinu ya maji ili mradi huo uweze kuwa endelevu kwa manufaa ya wananchi wenyewe.
No comments:
Post a Comment