Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, July 1, 2012

88 WAKAMATWA KWA UHALIFU MBEYA WANANCHI WAOMBWA KUJA TAMBUA MALI ZAO WALIZOIBIWA

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani akiongea na waandishi wa habari
 Pikipiki tatu zilizoibwa  namba T 584 BPU aina ya Star,T 301 BRU aina ya SanLG na T 489 BQU aina ya Sanya.
Kamanda Diwani akionyesha bunduki walizokamata



WATU 88 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uharifu ikiwemo wizi wa mafuta aina ya diseli kwaajili ya kuendeshea mitambo katika ujenzi wa barabara kati ya Tunduma-Sumbawanga.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani alisema watuhumiwa wa makosa hayo wamekamatwa katika oparesheni maalumu ya kupambana na uharifu iliyoanza Juni 8 mwaka huu.

Kamanda Amesema katika matukio ya wizi wa diseli jumla ya lita 4,440 zenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tisa zilikamatwa na tayari mahakama imeamuru mafuta hayo yarejeshwe yalikoibwa ili yakaendeleze shughuli za ujenzi wa barabara huku watuhumiwa nane wa wizi huo wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Lusekelo Paza,Anyemike Swile,Weiti Mwakatumbula,Michael Mwampamba,Mahona John,Erasto Mwaipaja,Seleman Nasoro na Hassan mrisho.

Amesema katika oparesheni hiyo pia zimekamatwa pikipiki tatu zilizoibwa akizitaja kuwa ni yenye namba T 584 BPU aina ya Star,T 301 BRU aina ya SanLG na T 489 BQU aina ya Sanya.

Mali nyingine ni bunduki mbili zilizotengenezwa kienyeji zinazotumia risasi za Shotgu,risasi nane,Televisheni mbili,kompyuta ndogo(Laptop) mbili,Printa moja,redio tatu,mbili aina ya Sub ufa na moja ya kawaida pamoja na simu nane za aina mbalimbali.

Hata hivyo amesema matokeo hayo mazuri yanatokana na ushirikiano mzuri ulioneshwa kati ya raia wema na askari wa jeshi hilo akisema wananchi walijitahidi kwa kiasi kikubwa kutoa taarifa juu ya uwepo wa vitendo vya uharifu.

Amewaomba wananchi kuendeleza ushirikiano huo mzuri akisema utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uharifu na kuufanya mkoa kuwa na amani na utulivu.

1 comment:

Anonymous said...

Kwanza nalipongeza jeshi na mamlaka husika kufanikisha kampeni hizo. Natoa shukrani za dhati kwa uibuaji wa wezi na mali zilizoibwa. Nipo morogoro lakini ninapoona huko mambo yanwekwa sawa kwa ushirikiano,huwa nafarijika. Asanteni. Man