Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, June 22, 2012

HIKI NI KAMA KICHEKESHO LAKINI PIA YASIKITISHA,UBISHI WACHANGIA PIA AJALI YA CANTER - MBEYA.


 Gari aina ya Canter Toyota ikiwa imetumbukia katika mto Jianga maeneo ya Ilolo Jijini Mbeya,  baada ya kuvunjika kwa daraja na katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa. Lakini wakazi wa eneo hilo walieleza kwamba daraja hilo ni bovu toka muda mrefu na viongozi wao hawajafanya jitihada zozote juu ya ubovu huo.
 Mmmh jamani hatari
Wakazi wa eneo la jirani na tukio la ajali waliofika kudhuhudia tukio hilo.

Hata hivyo kufuatia tukio hili,Kata za Ilemi,Sinde na Isanga zinapaswa kukutana katika meza moja ya mazungumzo kwa ajili ya kujenga daraja hilo ambalo ni kiunganishi cha kila pande na mara nyingi limekuwa likitumiwa na wagonjwa kwenda Kituo cha Afya cha Mwanjelwa na katika shughuli mbalimbali za kitaifa za kimaendeleo.
( picha na Godfrey Kahango).

1 comment:

Festo shempemba said...

Ugonjwa mkubwa unaowamaliza watanzania hawako tayar kutafuta chanjo wao wanaangalia tic baada ya ugonjwa kutokea.