Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, June 13, 2012

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA IMESAINI MKATABA WA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BOMBA.


Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo imesaini mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya bomba unaofadhiriwa na Benki ya Dunia utakaojengwa katika Kata ya Itagano Jijini hapa. 

Mkataba wa ujenzi wa mradi huo umesainiwa baina ya Meya wa Jiji Athanas Kapunga kwa niaba ya Halmashauri, na Kampuni ya Geotech Resources Employment and Development LTD(GRED) ya Jijini Mbeya.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Seko Nkusa amesema kuwa mradi huo utagharimu  shilingi milioni 293 nukta tano ambapo amepewa kampuni ya GRED kutandaza miundombinu ya bomba katani hapo baada ya kutimiza vigezo vya zabuni hiyo.

Nkusa amesema pamoja na kuwepo kwa mkandarasi huyo kutakuwepo na Mhandisi Mshauri ambaye ni Kampuni ya COWI ya Jijini Dar es Salaam ambayo itasimamia ukamilikaji wa mradi huo kwa gharama ya shilingi milioni 29 nukta mbili.

Aidha, amesema  mara baada ya kutia saini kwa mkataba huo mkandarasi atapewa siku 14 za kujiandaa na kutakiwa kukabidhi mradi huo kwa Halmashauri  baada ya miezi sita.

No comments: