SERIKALI Mkoani Mbeya, imesema hakukuwa na sababu yeyote ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo kutangaza kujiudhuru wakati tayari alikuwa na taarifa ya jina lake kutokuwepo kwenye orodha mpya itakayotangazwa na Rais.
Akitoa kauli hiyo jana kwa waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alisema serikali inashangazwa na kitendo cha kiongozi huyo kutangaza kujiuzuru wadhifa wake iliari alikuwa na taarifa ya kutochaguliwa tena na Rais Jakaya Kikwete.
"Kimolo alinifuata siku ya tarehe 24 Machi mwaka huu na kunieleza kuwa amepata taarifa ya kuwa jina lake halitakuwepo kwenye orodha mpya ya wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Rais sasa nashangaa uamuzi wake wa kuamua kujiuzuru
Alisema, Kwa mujibu wa Kimolo inasemekana alipata taarifa hiyo Mach 23 mwaka huu kutoka idara husika ikimueleza kuwa katika uteuzi mpya wa wakuu wa wilaya jina lake halitakuwepo.
Alisema, ndipo alipofika kwenye ofisi yangu na kunipa taarifa hiyo huku akilalamika sana kwanini jina lake lisiwepo wakati yeye ni mtendaji mzuri kwa Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Mkuu huyo alisema kitendo cha Kimolo kutangaza kujihudhuru ni kujikosha kwa jamii ili isishangae mara Rais atakapoteua wakuu wapya.
Pia, alimtaka kukubali matokeo na kwamba isifike sehemu kuanza kutafutana ubaya na watu na kwamba ni vema akaondoka kwa amani na upendo.
Hata hivyo alimtaka kuacha kuyaingiza makampuni makubwa kwamba yanamuandama yeye na kumsababishia awe na utendaji kazi mdogo unaopelekea yeye kujihudhuru.
3 comments:
Haya sasa makubwa.
Naomba nimrekebishe mwadishi...si kujiudhuru bali ni kujiuzulu
Propaganda za wana magamba,kwao kujiuzulu ni kusaliti umagamba(ccm).kandoro hujanena
RC asitake kutoa majibu mepesi ya kujiridhisha na kudanganya waTanzania. Ni kweli Mbozi kuna tatizo sana katika suala la ununuzi wa mazao na serikali imeshindwa kulitatua.
Binafsi nampongeza Kimolo kwa sababu mfumo wetu wa uongozi haumpi DC nafasi kubwa ya kuiongoza wilaya ya kuiongoza wilaya yake, zaidi anakua kama kikaragosi tu. Sasa kama ameona anasumbuliwa akaachia ngazi kwa nini Kandoro anataka kuleta uongo wa kitoto? Pia hapa kandoro anatoa siri ambayo sidhani kama wananchi tulitakiwa kuijua!
Post a Comment