Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, April 16, 2012

Wakazi Jijini Mbeya waomba Halmashauri ya Jiji Huduma ya Choo eneo wanapo fanyia maziko, Wadai wanalipia kiasi cha Laki nne kupata nafasi ya kuzikia Saba saba

 Haya ni baadhi ya makaburi eneo la saba saba Jijini Mbeya 
 Makaburi yakiwa yamejaa magugu huku hakuna mtu yoyote ambae anayatazama ama kuja kuyatoa na wengine wamepanda mazao yao maeneo hayo
 Ukuta huu ndio unatumika sasa kwa ajili ya huduma ya choo, kama unavyo unekana kubabuka ni kwa ajili ya Haja ndogo
 Hilo ni eneo la makaburi ambapo wakazi wengi Jijini Mbeya hulitumia kwa ajili ya maziko
Magugu yakiwa yameota eneo la Makaburini

********
Na mwandishi wetu maalum
Wakazi wa jiji la Mbeya wameiomba Halmashauri ya jiji la Mbeya kuwajengea choo sehemu ya mapumziko wakati wamazishi katika makaburi ya eneo la Saba saba, kwani wamedai ya kwamba wanalipa kiasi cha shilingi laki nne (400,000) kwa kipande kidogo sana cha kuzikia. 
Pia wamelaani vikali Halmashauri hiyo ya jiji  pamoja na kulipwa fedha nyingi lakini hawajali wala Kuthamini eneo hilo jambo lililo sababisha eneo hilo kujaa vichaka na Magugu mengi.
kukosekana kwa Choo katika eneo hilo kumesababisha wananchi kujisaidia kiholela holela katika kuta za uzio wa makaburi hayo.
Katika swala  hilo pia wakazi wa Jiji la Mbeya wamehoji maswali mengi ikiwa na Je Pesa wanazo lipia makaburini hapo huwa zinafanya kazi gani? wamedai kwamba wanaona hazifanyi kazi yoyote zaidi ya kumkuta muhusika anae elekeza eneo la kufanyia maziko na kukabidhiwa Risiti ya malipo ya  eneo husika ya hapo walipo nunua yani shilingi laki nne.
Pamoja na hayo yote wakazi wa jiji wanaiomba Halmashauri ya Jiji kujenga uzio imara kwa sababu baada ya mazishi kufanyika vibaka huja eneo hilo wakiiba mashada na hata kufukua makaburi hayo pindi wanapo ona Marehemu alikuwa na uwezo na inawezekana amezikwa na Vito vya Thamani.

No comments: