Mche uliathiriwa na ugonjwa unaoozesha mashina na mizizi unaitwa sterm and root rot unasababisha virusi vya vimelea vya Emilea melea vinavyoangamiza kabisa mimea ya kahawa na kuwa mikavu kabisa kama kuni.
Mtafiti kutoka TACRI Bwana Dismas Pancras, akishika mche ulioathirika na ugonjwa unaoozesha mashina na mizizi unaitwa sterm and root rot unasababisha virusi vya vimelea vya Emilea melea vinavyoangamiza kabisa mimea ya kahawa na kuwa mikavu kabisa kama kuni.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mtafiti wa zao la Kahawa kutoka Chuo cha Utafiti nchini (TACRI), Mbamba, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Bwana Dismaas Pancras, amewataka wakulima wa zao hilo kuchukua tahadhari kufuatia ugonjwa hatari ulioingia kushambulia kwa kasi miche ya zao hilo.
Ametoa angalizo hilo katika moja ya Kata zilizotembelewa katika mfulululizo wa ziara yake ya mafunzo kwa kata zote zinazostawisha zao hilo wilayani humo.
Ameongeza kuwa ugonjwa huo unaoozesha mashina na mizizi unaitwa sterm and root rot unasababisha virusi vya vimelea vya Emilea melea vinavyoangamiza kabisa mimea ya kahawa na kuwa mikavu kabisa kama kuni.
Bwana Dismas amesema ugonjwa huo hauna tiba kabisa hivyo amewataka wakulima pindi mashamba yao yanapokuwa na ugonjwa huo ni vema kuing’oa kabisa miche hiyo na kuiteketeza, kwa moto pia kufukia mashimo hayo baada ya kuweka chokaa mashimoni na kuyapumzika miaka mitatu mashamba yaliyoathiriwa na ugonjwa.
Miongoni mwa wakulima walioathirika na ugonjwa huo ni pamoja na Bwana Aloyce Mdalavuna wa kata ya Bara, kwani baadhi ya miche ya zao la kahawa imekufa baada ya kukumbwa na ugonjwa huo hatari.
Ugonjwa huo hupendelea zaidi sehemu yenye ukame ambapo katika wilaya ya Mbozi ni Kata ya Bara na Kata ya Ipunga, na kwamba wakulima wanatakiwa kuchimba mabwawa ya kuhifadhi maji ili kusaidia kumwagilia wakati wa ukame na kutokomeza ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment