Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, April 6, 2012

MADIWANI WAPITISHA BAJETI YA WILAYA YA MBOZI - MBEYA NA WAAMBIWA WAACHE TOFAUTI ZAO

Mkuu wa wilaya ya Mbozi GABRIEL KIMOLO akifungua mkutano wa baraza la madiwani Mbozi

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi ERICK MINGA AMBAKISYE 
 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI LEVISON CHILLEWA AKITOA UFAFANUZI JAMBO KWENYE KIKAO HICHO





Baraza la Madiwani wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya limefanyika Aprili 5 mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, kwa ajili ya kujadili mapato na matumizi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/2012 na kupitisha bajeti ya 2012/2013.

Baraza hilo lilifunguliwa na Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Gabriel Kimoro, ambapo amesema kuwa madiwani waondoe tofauti zao za kisiasa kwa nia ya kuijenga wilaya hiyo na kuleta maendeleo.

Aidha mkutano huo ulipitisha bajeti ya shilingi bilioni 2.5, kwa ajili ya mendeleo ya elimu, miundombinu na afya, hivyo madiwani wametakiwa kusaidia kukusanya mapato hayo ili asilimia fulani irudi kwenye kata zao kwa lengo la kuleta tija ya maendeleo kwa wilaya hiyo.

Naye, Mwenyekiti wa halmashauri wa Mbozi ambaye pia ni mwenyekiti wa mkutano huo Mheshimiwa Erick Ambakisye, amewasisitiza madiwani kutofumbia macho pindi wanapoona watendaji wa halmashauari kwa kushirikiana na mawakala hawakusanyi ushuru ipasavyo.

 Hata hivyo madiwani nao wamesema kutokana na makisio madogo wanayopewa na halmashauri wamekuwa hawatozi ushuru sahihi wa mazao, kwa magari yanayochukua mazao kutoka wilaya hiyo na kujinufaisha binafsi kwani kwa kufanya hivyo ni kuikosesha Serikali mapato.

Wakati huo huo bajeti hiyo ilisomwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Bwana Levison Chilewa, ambapo awali aliwasilisha bajeti ya bilioni 2.2 ambayo ilikataliwa na madiwani na kuongeza bilioni 2.2 hadi 2.5.

Wameongeza kuwa kuna vyanzo vingi vya mapato kama vile zao la kahawa, ufuta na mazao mchangantiko ya nafaka na biashara ambayo yanalimwa wilayani humo.

Mwenyekiti wa mkutano Bwana Erick aliwattuliza jazba madiwani baada ya diwani wa Kata ya Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka alipoinuka na kusema anawapongeza wananchi wa Arumeru kwa kumchagua mbunge wa CHADEMA, hali iliyopelekea Mwenyekiti wa mkutano kumkanusha kwa hapo wanajadili masuala ya maendeleo ya wilaya ya Mbozi na sio Jukwaa la siasa, mbona hakusema Lema alivyovuliwa ubunge, ambapo madiwani waliangua kicheko.

Mkutano huo ulimalizika kwa Mwenyekiti kuwataka madiwani kukutana Aprili 20 mwaka huu ili kujadili marekebisho ya bajeti hiyo.

Mbali na upitishwaji wa bajeti hiyo, madiwani hao walimlaumu Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde kwa kudhohofisha maendeleo katoka jimbo lake kutokana na kuwaambia wananchi wake wachangie shilingi  2,500 kwa ajili ya ujenzi wa shule ambazo hazitoshi kutokana na gharama za ujenzi kupanda 


 
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya

1 comment:

H.Mwamatandala said...

Naomba uniwekee swala hili niweze kujua hasa wana Kyela,mimi napenda kujua ni kwa nini wilaya ya Kyela mvua hunyesha wakati wa usiku tu,mimi ni mwenyeji wa kyela kidogo, ningependa kujua mengi ambayo sikuyajua huko nyuma?wengi watakubaliana na mimi kuhusu hili.