Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 15, 2012

WAMACHINGA JIJINI MBEYA WAZIDI KUJIMILIKISHA MAENEO KATIKATI YA JIJI HUKU JIJI LIKIWA LINAWATAZAMA TU KAMA SHERIA HAKUNA

Ofisi ya TRA mkoa  wa Mbeya uzio wake ukiwa umepambwa na mataulo ya wamachinga hao huku mamlaka husika zikiwatizama tu wamachinga hao bila ya kuwachukulia hatua yeyote
Barabara ya kuingia katikati ya jiji la mbeya pembeni ya jengo la TRA mkoa wa Mbeya wamachinga wapo huru kabisa huku waenda kwa miguu wakipita barabara ya magari kana kwamba hawana njia yao ya kupita mambo hayo ya jiji la mbeya sijui nani anaeusika kwa hili
Nani hatua chache sana kufika katika ofisi kuu za halmashauri ya jiji la mbeya na ni jia kuu ya kupita viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika barabara hii je haya ni mapambo?
Ofisi za TRA mkoa wa Mbeya zikiwa zimezungukwa na badhaa mbalimbali za wamachinga hao
Cha ajabu mgambo wa jiji wanahangaika na vijana waosha magari mjini huku wamachinga wakiwaacha wakichafua mji kwa kupanga vitu vyao kiholela tena katikati ya mji na ofisi kuu za serikali na taasisi kubwa za kibenki 

1 comment:

Anonymous said...

Hivi ngoja nihoji nyie mbeya yetu mmetumwa au?sasa kwa kupanga vitu vyao mbele ya benki au mbele ya jengo inaathiri nini? na kiuchumi ni kawaida kwamba kukiwa na taasisi kubwa ya kiuchumi basi inavutia taasisi zinginezo ndo kanuni za uchumi ndo uchumi unavyofanya kazi.......na haya mambo ya kuwafukuza watu maeneo yao ya biashara yameletwa na watalii wa magharibi na watu paranoid ambao wanadai kwamba miji isipokuwa na mpagilio basi inasababisha hatari na ugaidi sasa na nyie mbeya yetu mnaongea kitu hicho hicho kisicho na manufaa kwenu wala kwa wana mbeya