Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, March 28, 2012

MTUHUMIWA ALIYETOROKA MAHABUSU AKAMATWA


Kituo cha Polisi Kati kilichopo Jijini Mbeya.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Maneno Wiwa Kalinga mmoja wa mahabusu waliotoroka wiki iliyopita katika Kituo cha Polisi Kati, Mkoani Mbeya amekamatwa akiwa mafichoni Wilayani Mbozi.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa majira ya saa 10 alfajiri katika kijiji cha Ruanda wilayani humo.

Kukamatwa kwake kumetokana na msako mkali uliofanywa na Jeshi la polisi  mkoani hapa, mara baada ya kutoroka kwa kuchimba ukuta wa Kituo hicho.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi, amethibitisha kukamatwa kwa mahabusu huyo na kufanya jumla ya waliokamatwa kufikia wawili, huku mwenzake  Fadhili Mwaitebele (27) makazi wa Ilomba jijini Mbeya alikamatwa muda mfupi baada ya kutoroka.

Hata hivyo Kamanda Nyombi ametoa wito kwa wananchi kuwa popote watakapo waona wahalifu hao watoe taarifa kituo chochote cha Polisi kwani watu hao ni hatari katika jamii.

No comments: