Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, March 20, 2012

Live: Tukio zima la Ajali mbaya la basi la Prince Muro iliyo tokea jana Usiku maeneo ya Senjele likielekea Tunduma. Mwendo kasi ndio chanzo cha ajali hiyo mmoja Afariki 14 majeruhi

Basi la Price Muro Baada ya kupata ajali usiku wa kuamkia jana likielekea Tunduma kutokea Dar es salaam.

Likiwa linaonekana baada ya kupinduka 

Hivi ndivyo zinavyo onekana Damu na viti kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo iliyo tokea jana usiku

Baadhi ya mabaki ya vitu baada ya ajali hiyo jana usiku

Hili Ndilo Gari la mizigo ambalo basi la Price muro lilitaka kulipita, na  baadae kushindwa na kupinduka baada ya kukutana na Gari lengine mbele yake


Shimo hili limechimbika wakati wa ajali hiyo ilipo tokea jana usiku

Hapa ndipo Basi la Prince Muro lilipo taka kuingia na kulikwepa gari hili na kupindukia upande wa pili 

Muonekano wa gari hili la mizigo ambalo limeharibikia bara barani 

Mmoja wa majeruhi ambae alikuwa anatokea Dar es salaam kwenda kuwasalimu ndugu zake Ileje aliye fahamika kwa jina moja tuu la Andendekisye akiwa katika Hospital ya Ifisi Mbeya Muda huu

Baadhi ya Majeruhi walio nusurika katika ajali hiyo wakiwa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea katika matibabu na kutazamwa kama wamepata matatizo yoyote.

Hawa ni majeruhi kati ya wale 14

Mganga mkuu wa Hospitali ya Ifisi Dkt. Mbilinyi akiongea na moja ya majeruhi mapema leo.

Majeruhi ambao wamenusurika katika ajali hiyo mbaya wamesema kwamba dereva huyo alikuwa mwendo kasi tangia walipo fika mikumi, Wameendelea kudai kwamba walimpa onyo mala kadhaa lakini hakuweza kuwasikiliza na akaongeza mwendo kasi zaidi mpaka walipo pata ajali hiyo maeneo ya Senjele kuelekea Tunduma.
Habari kamili itakuja mpaka sasa kuna majeruhi 14 na mtu mmoja amefariki Dunia


2 comments:

mpoki said...

poleni watu wote mlio pata ajari na kuhumia au kupoteza mali zenu
pole kwa ndugu wa marehemu kwa kupoteza ndugu yao
Ila tukiachia uzembe na mwendo kasi wa mabasi yetu haya lakini mimi naona maloli yamekuwa ni chanzo kikubwa sana cha Ajari nyingi sababu yakiharibika huwa hayatolewi barabarani mbya zaidi hata halama mengine huwa hayaweki sasa na hizi barabara zetu nyembemba inakuwa shida sana

mie cha kuomba ndugu zetu madereva wa maloli yakiharibika basi waweke alama za kutosha kuanzia mbali na ikiwezekana wayatoe barabarani kabisa

MUNGU BARIKI TNZANIA MUNGU BARIKI AFRICA

Anonymous said...

Natoa pole kwa wote walioathirika katika ajali hii. Haya maelezo kuwa basi lilipata ajali lilipojaribu kulipita lori yanakanganya kwa sababu picha zinaonyesha magari hayo yalikuwa katika muelekeo tofauti yaani basi lilikuwa likienda Tunduma na lori lilikuwa likitoka Tunduma. Kwa hiyo insingewezekana basi kulipita lori lililokuwa linaelekea upande mwingine. Nadhani kilichotokea hapa ni lori hilo liliharibika katikati ya barabara na kuachwa hapo na wakati basi lilipokaribia sehemu hiyo kulikuwa na gari lingine lililokuwa linalikwepa lori hilo. Hii ilimlazimu dereva wa basi atoke barabarani kuepuka kugongana na gari hilo.