Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mwalimu wa shule ya msingi Bwato wilaya ya Kyela mkoani mbeya Bwana Herny Hans Mwaikokoba anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, mwenye umri wa miaka 13.
Tukio hilo likiwa ni la pili kwa mwalimu huyo kumtendea mtoto huyo, ambalo limethibitishwa na mtoto mwenyewe na shangazi yake aitwaye Bi Sabina Ndobo mkazi wa kijiji cha Bwato wilayani humo.
Mara ya kwanza mnamo Oktoba mwaka uliopita, mwalimu huyo alimtendea tukio hilo la kumbaka mtoto huyo na kisha kumpa shilingi 200, ili anunue mihogo na tukio la pili alilifanya Novemba mwaka uliopita ambapo alimpa shilingi 500, baada ya mtoto huyo kupiga kelele na kijana aliyekuwa akikaanga mihogo Bwana Mwarabu alimuokoa mtoto huyo.
Wakati mwalimu huyo akitenda kosa hilo alimtishia kumfukuza shule au kumuua mtoto huyo endapo atatoa siri hiyo.
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo ya msingi, Bwana Benjamin Mwailomo alipewa jukumu na walimu akabidhi shilingi 250,000 kwa mzazi ili suala hilo asilipeleke Polisi, lakini mwenyekiti huyo na bodi yake walitaka kumkabidhi mzazi shilingi 200,000 ambapo alizikana na kuwarudishia.
Baada ya mzazi kugoma ndipo walimu hao walichukua jukumu la kumuita mzazi na kumkabidhi pesa hizo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bwana Hussein Mwakifumbwa Anangisye amekanusha kutokea kwa tukio hilo, ingawa ametajwa na mtoto huyo mara kadhaa kuhusika katika vikao vya usuluhishi wa suala hilo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwana Alfredy Kalapila (55) na Mwenyekiti wake Bwana Peter Bahesya Mwakisomola (40), wamesema watalifuatilia suala hilo na kulifikisha katika kikao cha bodi ya shule siku ya Ijumaa.
Hata hivyo wazazi wa mtoto Bwana Kambona Petro Mwangomo amesema ameshawahi kumpeleka mtoto huyo katika zahanati kwaajili ya vipimo ambapo hakuweza kubainisha mara moja vipimo vilisemaje.
Mtandao huu umebaini kuwepo kwa kiini macho cha tukio hilo la ubakaji ambapo mwenyekiti wa bodi ya shule Bwana Mwailomo kukiri mtoto huyo kutendea ubakaji na mtu mwingine aitwaye Natron Mwaisumo (50) ambaye amedai ametoroka kijijini hapo, kitu ambacho kimegunduliwa na mtandao huu kuficha uovu uliofanywana mwalimu ili hatua za kinidhamu na kisheria zisichukuliwe.
Je? Asasi za zinazolinda haki za watoto ziko wapi?......
No comments:
Post a Comment