Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, February 17, 2012

MAHALI AMBAPO KABULI LILIFUKULIWA NA MWALIMU WA SHULLE WA MSINGI AKISHIRIKIANA NA MGANGA WA KIENYEJI - KYELA.


Mwenyekiti wa kijiji cha Bwato wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Bwana Nicodemus Mwakasungula (41), akionesha eneo ambalo kaburi la Marehemu British Mwamiko aliyefariki Februari 2010, na kaburi hilo kufukuliwa na mdogo wake Mwalimu Yusuph Mwamiko (55) wa Shule ya msingi Isimba iliyopo Kijiji cha Masoko, Kata ya Makwale wilaya huo kwa kushirikiana na Mganga wa Kienyeji ambapo tukio hilo ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.
"YESU NI BWANA" ni neno lililoandikwa katika Mlango wa nyumba ya Mwalimu Yusuph Mwamiko (55) wa Shule ya msingi Isimba iliyopo Kijiji cha Masoko, Kata ya Makwale wilaya ya Kyela mkoani Mbeya aliyefukua kaburi la marehemu kaka yake kwa kushirikiana na mganga wa kienyeji kwa madai ya marehemu alizikwa na vitu katika miguu yake, ambayo ilivikwa viatu, na vitu ambavyo vilikuwa vinasababisha ugumu wa maisha (kiuchumi) na pia kuleta vifo katika ukoo wao na mpaka sasa watu 9 wamefariki hivyo kuzua hofu katika ukoo wao.
Pichani ni nyumba inayomilikiwa na Mwalimu Yusuph Mwamiko (55) wa Shule ya msingi Isimba iliyopo Kijiji cha Masoko, Kata ya Makwale wilaya ya Kyela mkoani Mbeya aliyefukua kaburi la marehemu kaka yake kwa kushirikiana na mganga wa kienyeji kwa madai ya marehemu alizikwa na vitu katika miguu yake, ambayo ilivikwa viatu, na vitu ambavyo vilikuwa vinasababisha ugumu wa maisha (kiuchumi) na pia kuleta vifo katika ukoo wao na mpaka sasa watu 9 wamefariki hivyo kuzua hofu katika ukoo wao.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwato anayofundisha Mwalimu wa shule ya msingi Bwato wilaya ya Kyela mkoani mbeya Bwana Herny Hans Mwaikokoba anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, mwenye umri wa miaka 13, ambalo ni tukio la pili kwa mwalimu huyo kumtendea mtoto huyo, ambalo limethibitishwa na mtoto mwenyewe na shangazi yake aitwaye Bi Sabina Ndobo mkazi wa kijiji cha Bwato wilayani humo.

No comments: