Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, December 29, 2011

Wazazi kulalamika hali ngumu ya maisha yachangia watoto kuishi katika mazingira magumu

 Watoto wadogo wenye umri chini ya miaka 15 wakiwa maeneo ya Uhindini Jijini Mbeya wakiwa wanacheza kamali wakati wanangojea kupata chochote.
 Haya ni Baadhi ya Magari ambayo yameegeshwa eneo la TRA ambapo watoto hawa huanza kuyaosha hata kabla ya kuambiwa, na Baadae kufanyiwa malipo kama mwenye usafiri atalidhika

 Kijana Mdogo John akiwa anaosha Gari eneo hilo ambapo hakuambiwa afanye hivyo lakini alilazimika ili apate chochote
 Vijana wadogo wakiwa wanacheza kamali na kutaka kupigana Baada ya mwenzao kuonekana kushinda na kudai ni mdhurumaji.

Kijana John akionekana kuelekea Kuchota maji machafu ya mtaloni ili aweze kumalizia kusafisha Garialilo kuwa akiliosha.
*********************
Katika pita pita zetu leo Kamera yatu imefanikiwa kuwanasa watoto ambao walikuwa wanaonekana wako bize kungojea magari kuegeshwa ili wapate kuyaosha na kupata chochote, Mwandishi wetu maalum ambae alikuwa akiwafuatilia kwa umakini watoto hawa na kupata nafasi ya kuwahoji mmoja baada ya mwengine, wengi wao walidai ya kuwa hali ngumu ya maisha na wazazi kulalamika hali ngumu ya maisha ndivyo viliwasababisha wafanye hivyo. 
Hata hivyo baadhi ya watoto wamesema kwamba wanafanya hivyo ili kutafuta ada ya shule na kununua mavazi na viatu pia kupata pesa za kula.
Vijana wengine wawili wamedai ya kwamba wameachishwa masomo ili wasaidie wazazi wao kupata chochote cha kula ikiwa wenyewe ni wazima hawana ulemavu wowote lakini hawataki kujihusisha na maswala yoyote yale hata kazi ndogo ndogo.
Mwisho vijana hao wadogo wamedai kuwa Serikali iwaangalie na ikiwezekena wazazi wao wapewe adhabu kubwa ili iwe Fundisho kwa wazazi wengine ambao hawana ulemavu wa aina yoyote lakini ni wavivu na kushinikiza watoto wao wafanye kazi izo ambazo zipo katika mazingira magumu na pengine kuwasababishia kuwa wezi ama machokoraa.


1 comment:

Anonymous said...

hao ndo majambazi wa kesho