Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, December 10, 2011

WAFANYABIASHARA WATATU WAKAMATWA KWA MAUAJI YA MUUZAJI NA MTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA


POLISI Mkoani Mbeya inawashikilia wafanyabiashara watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Fredy Manji (45) mkazi wa Mji mdogo wa Mbalizi ambaye aliuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Marehemu Fredy, mbali na kujishughulisha na kazi ya ukulima pia inasemekana ni mtumiaji  na muuzaji wa madawa ya kulevya.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na mbili alfajili katika eneo la Majengo lililopo  Mji mdogo wa  Mbalizi Mbeya vijijini.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Francis Mwakatika (38) mkazi wa Sokomatola, Thadei Abel (40) mkazi wa Mshikamano-Mbalizi pamoja na Mathar Thadei(35) mkazi wa Mbalizi ambao wote ni wafanyabiashara.

Alisema polisi walipata taarifa kuwa mwili wa marehemu Fredy umeonekana umetupwa kwenye eneo la majengo ukiwa na jereha kichwani ambapo askari walifika na kuchukua mwili huo.

Alisema, mwili huo ulifanyiwa uchunguzi na kukutwa na jereha kwenye kichwa chake lililotokana na kupigwa na kitu chenye kali na kusababisha kifo chake papo hapo.

Nyombi, alisema askari walifanya uchunguzi wao na kufanikiwa kukamata watuhumiwa watatu wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo na kwamba bado wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano.

Aidha, Kamanda Nyombi alisema  uchunguzi wa polisi umebaini kuwa marehemu Fredy alikuwa akijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na alikuwa akitumia madawa hayo.

Hata hivyo, alisema mwili wa marehemu Fredy umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya na kwamba watuhumiwa wote watatu watafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapo kamilika.


No comments: