Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, December 22, 2011

VODACOM FOUNDATION YAWAJALI WATOTO YATIMA MBEYA

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Evans Balama akikabidhi vifaa vya shule kwa watoto yatima na wenye uhitaji maalum wa mkoani Mbeya, vilivyotolewa na kampuni ya simu ya Vodacom kupitia kampeni yake ya Share&Care. Jumla ya watoto 500walinufaika na msaada huo ambapo pia vituo 15 vya kulelela watoto hao vilipatiwa vyakula katika hafla iliyoambatana na chakula cha mchana. Kulia ni Mkuu wa mfuko wa Jamii wa Vodacom, Yessaya Mwakifulefule na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga. 
wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom mkoani Mbeya wakijumuika pamoja na watoto yatima na waishio katika mazingira magumu kucheza muziki mara baada ya kupata chakula cha mchana na watoto hao pia kukabidhi zawadi za vyakula na vifaa vya shule kwa ajili ya krismasi kwa watoto hao zaidi 500 mwishoni mwa wiki. Hafla hiyo ni mwendelezo wa kampeni ya Vodacom Share & Care ambayo imegharimu zaidi ya shilingi milioni 50 kwa mikoa mitano. 
Moja kati ya wafanyakazi wa vodacom akiteta na mmoja ya watoto yatima
pamoja na baadhi ya wazazi na walezi wa vituo vya yatima vya mjini Mbeya kwa kuwahudumia. Vodacom kanda ya kusini mwishoni mwa wiki iliandaa tafrija kubwa ya chakula cha mchana kwa watoto yatima zaidi ya mia tano ambao pia walipatiwa zawadi za vyakula kwa ajili ya vituo vinavyowalea, sare za shule na vifaa mbalimbali vya shule kupitia kampeni ya Vodacom Share& Care.
Watoto hao pia walionyesha umahili wao wakucheza ngoma ya  mganda kwa step

No comments: