Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, December 12, 2011

MAUAJI YA KUTISHA MBARALI

Mwanakijiji wa Kijiji cha Mahango Kata ya Ruiwa Wilayani Mbarali, Mensadik Mbembela akionesha kaburi la marehemu Bariki Sanga baada ya mwili wake kuopolewa Chooni ukiwa umenyofolewa baadhi ya viungo vyake vikiwemo Sikio, Ulimi na sehemu za Siri. Kufuatia kuharibika vibaya kwa mwili huo ililazimika kuuzika kandoni mwa nyumba iliyo karibu na choo kilichokutwa mwili huo.Jeshi la Polisi Wilayani humo linawashikilia watu wanne kwa kuhusika na mauji hayo.
*****
Habari na Picha na Ezekiel Kamanga, Mbarali
Bariki Sanga mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Uyole jijini Mbeya ambaye alikuwa akifanya biashara ya ulanguzi wa mpunga katika kijiji cha Wimba mahango kata ya Igurusi amekutwa akiwa amefariki dunia ndani ya shimo la Choo huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya.

Mwili wake umekutwa ndani ya choo ukiwa umewekwa kwenye gunia na kufungwa na nguo mbalimbali jana majira ya saa kumi za jioni baada ya ndugu na marafiki kumtafuta kwa zaidi ya wiki moja.

Kutokana na tukio hilo mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Witson Kazimoto amewataka wananchi wa kijiji hicho washirikiane na Jeshi la polisi ili kuweza kumpata Bariki Mbariko ambaye anadaiwa kuwa mara ya mwisho alikuwa na marehemu na walikuwa wamekubaliana kwenda kulangua mpunga.

Inadaiwa kuwa marehemu huyo alikuwa na fedha taslimu shilingi laki sita na alizikwa jana usiku jirani na eneo alilokutwa kutokana na mwili wake kuharibika vibaya hivyo kushindikana kusafirishwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa hadi sasa Jeshi la polisi linawashikiria watu wawili kwa kuhusika na tukio hilo.

No comments: