Askari Mary Gumbo ambaye ni katibu wa mtandao wa wanawake wa Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya akikabidhi mche wa sabuni kwa mmoja wa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima kinachoitwa Simike kinacholelewa na Mama Anna Kasile.Kituo hicho kina jumla ya matoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi 108.
Askari Mary Gumbo ambaye ni katibu wa mtandao wa wanawake wa Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya akikabidhi katoni ya sukari kwa Bwana Thomas Msifuni ambaye analelewa katika kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kinachoitwa Simike kinacholelewa na Mama Anna Kasile. Kituo hicho kina jumla ya matoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi 108.
Askari kutoka Jeshi la Polisi mkoani Mbeya ambao wanafahamika kama Mtandao wa wanawake wa Jeshi hilo wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima kinachoitwa Simike kinacholelewa na Mama Anna Kasile.Kituo hicho kina jumla ya matoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi 108.
Baadhi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kati ya watoto 108 wanaolelewa na kituo cha Simike kinachosimamiwa na Mama Anna Kasile, wakiimba wimbo kuwakaribisa Askari wa mtandao wa wanawake kutoka Jeshi la Polisi mkoani Mbeya.
Baadhi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kati ya watoto 108 wanaolelewa na kituo cha Simike kinachosimamiwa na Mama Anna Kasile, wakiwa wameketi chini wakisubiri kupewa misaada kutoka Kwa Askari wa Mtandao wa Wanawake kutoka Jeshi la Polisi mkoani Mbeya..
HITIMISHO:-
Jeshi la polisi kupitia Askari wa mtandao wa wanawake mkoani Mbeya wamekabidhi misaada yenye thamani ya zaidi ya shilingi 500,000/= wa nguo, sabuni, sukari, daftari na chakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Simike kinachosimamiwa na Mama Anna Kasile.
Akikabidhi misaada hiyo Katibu wa Mtandao huo Kopro Mary Gumbo amesema wametoa msaada huo ili kuwatia moyo watoto hao ili waweze kupata chakula na kuwawezesha kupata elimu.
Ameongeza kuwa Taasisi, mashirika na wadau mbalimbali wanatakiwa kuchangia vituo vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ili kuweza kuondoa wimbi la watoto wa mitaani.
Kopro Mary amesema Mtandao wao upo nchini kote wenye lengo la kuwaondolea wanawake changamoto wanazokutana nazo kama kutelekezwa, kunyanyapaliwa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto na akina mama.
Kwa upande wake mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho Thomas Msifuni ametoa shukrani kwa mtandao na kuwaomba wazazi, Taasisi na mashirika kuiga mfano wa Mtandao huo kwani wanajisikia kuwa na wazazi ambapo wameahidi kusoma kwa bidii.
Hata hivyo Mlezi wa kituo hicho Mama Anna Kasile ameomba msaada wa hali na mali uendelee kutolewa ili kuweza kumudu gharama za kuendeshea kituo hicho na kwamba hana mfadhili yeyote kwani anawategemea wasamalia wema na wakati mwingine hudiriki kuuzamali zake ili kumwezesha kupata ada za baadhi ya watoto ambao huwalea kwani wengi wao wanasoma Shule za Sekondari.
No comments:
Post a Comment