Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 2, 2011

WANAFUNZI 138 WA SHULE YA MSINGI WALAZIMIKA KUSOMA KATIKA DARASA MOJA - MBEYA


Na mwandishi wetu
Wanafunzi wa shule ya msingi Tambukareli iliyopo kata ya Itezi Jijini Mbeya wanalazimika kusoma wanafunzi 138 katika chumba kimoja cha darasa kutokana na uchache wa vyumba vya madarasa.
Wakati sera ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaagiza wanafunzi 45 kusoma katika katika darasa moja.
Hayo yamebainika baada ya kada mmoja wa Chama Cha Mapinduzi mkoani hapa Shambwee Shitambala kuitembelea shule hiyo na kuangali mazingira ya shule.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Boniphace Mwakyelu, amesema shule hiyo inajumla ya wanafunzi 825 na inaupungufu wa vyumba vya madarasa 15 ambapo hivi sasa shule hiyo inavyumba 6 vya madarasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Itezi, Peter Ringo, amesema matatizo yanayoikabili shule hiyo yanaweza kutatuliwa endapo baadhi ya viongozi wa kata hiyo wanaweza kuondoa itikadi za kisiasa katika utendaji kazi.
Kwa upande wake Shitambala alichangia shilingi laki 6 ili kutoa msukumo kwa wananchi wa kata hiyo kujitoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule na kuwasihi viongozi kuondoa itikadi za kisiasa katika utekeleza wa mambo muhimu ya kitaifa.

No comments: