Askali wa Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabara akikagua basi aina ya Scania yenye nambari za usajili T 207 BFJ mali ya kampuni ya Badget lililopinduka jana majira ya saa 12:30 asubuhi eneo la Mlimanyoka jini Mbeya ambapo zaidi ya abiria 50 wamenusurika kifo.
Abiria zaidi ya hamsini wamenusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya kampuni ya Badget lenye nambari za usajili T 207 BFJ aina ya Scania kupinduka .
Ajali hiyo imetokea majira ya saa kumi na nusu alfajiri baada ya basi hilo lililokuwa linaendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina moja la Bwana Mwamtobe lilipojaribu kuyakwepa maroli mawili yaliyokuwa yakipandisha katika mlima nyoka maeneo ya Uyole jijini MBEYA.
Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya ambapo hali zao zinaendelea vizuri,baadhi ya majeruhi ni Vumilia Maiko na Bwana Mateni Beni.
Mkuu wa usalama barabara Bwana Ezekiel Mgeni amewataka madereva kuwa makini wanapoendesha magari ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Bwana Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwaasa madereva kuwa makini.

1 comment:
Madereva kuwenia makini. Pole kwa majeruhi
Post a Comment