Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 30, 2011

SAKATA LA VURUGU ZA MBEYA ,MEYA ARUKA KIMANGA KUCHOCHEA VURUGU ZA WAMACHINGA MBEYA.


Na Francis Godwin


.Ashangaa chama chake kumgeuza mnyamwezi wa mizigo.

MEYA wa Jiji la Mbeya,Athanas Kapunga,ameibuka na kuwatupia lawama viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani hapa,kuwa wamekiuka taratibu na utamaduni wa chama, kwa kumhukumu bila kumpatia muda wa kujitetea,kufuatia chama hicho kutoa tamko linalowataja viopngozi waandamizi wa halmashauri hiyo kuwa ndio chanzo cha vurugu za wamachinga na polisi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 17 kujeruhiwa kwa risasi na Mabomu ya machozi.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa meya huyo Amesema badala yake viongozi hao wa CCM,ambaye yeye pamoja na nafasi yake ya umeya ni katibu mwenezi na Itikadi wa chama hicho ngazi ya wilaya ya Mbeya Mjini,walisukumwa zaidi na hisia binafsi za kisiasa na kuamua kumuhukumu bila kuwapatia nafasi.
Kapunga alitoa tamko hilo jana Jijini hapa,katika mkutano wa waandishi alioutisha kwa lengo la kujibu matamnko na tuhuma mbalimbali zilizotolewa na taasisi mbalimbali,ikiwemo CCM kulaani vurugu za wamachinga na polisi zilizoibuka Novemba 11 hadi 12 katika eneo la Mwanjelwa Jijini hapa.
Wiki mbili zilizopita halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mbeya ilikutana kwa dharura na kutoa tamko kali la kulaani vurugu zilizoibuka na bila kificho iliwatupia lawama viongozi waandamizi wa Halmashauri ya Jiji kuwa ndio chanzo cha vurugu kwa kuwalazimisha wamachinga kuondoka eneo hilo la Mwanjelwa bila kuwapa eneo mbadala.
Tamko hilo pia liliwataka viongozi hao wa Jiji kuhakikisha wanawadhibiti mgambo wa wake kwa kuwa wamekuwa wakiwanyanyasa wafanyabiashara hao kutokana na kuendesha uparesheni zisizo na mpangilio huku wakipora mali na bidhaa za wafanyabiashara hao.
Kapunga alisema “ mimi hapa Halmashauri ndio Kamisaa wa chama changu,wasingepaswa kunilaumu bali walitakiwa kuniuliza ,…CCM ni vikao ingeniita ,halmashauri kuu ni chombo kikubwa Mkuu wa wilaya ni mjumbe angeniita tu,Mkuu wa mkoa ni mjumbe na ndio kada mkuu wa chama alishatoa tamko juu ya kilichotokea,yeye alitosha kutubeba wote si wengine kuibuka kwa hisia zao tu ” .
Hivyo alisema anamini kuwa matamko hayo yalikuwa yawatu binafsi ndani ya chama chake kwa kuwa hayakuzingatia utaratibu wa chama wa kutoa adhabu bila kumpatia mtuhumiwa nafasi ya kujitetea.
Akiendelea kujibu maswali ya waandishi wa habari Meya Kapunga alishikwa na kigugumizi kwa kushindwa kumtaja mtu aliyetoa amri ya mgambo kwenda kufanya oparesheni ya kuwaondoa wamachinga ilihali tayari kulikuwa na mazungumzo baina yao na viongozi wa wamachinga.
“Waandishi wa habari kama hamjui mipaka ya utendaji ndani ya halmashauri ngoja niwaelimishe mimi kama Meya huwa natoa maelekezo tu kwa Mkurugenzi baada ya maamuzi kutoka ndani ya vikao vya baraza la madiwanisiwezi kwenda kuamuru mgambo wakafanye vurugu ” alisema .
Hata hivyo alitolea ufafanuzi kuwa maamuzi ya wamachinga kuondolewa katika eneo hilo la Mwanjelwa, lilifikiwa kwenye vikao vya baraza la madiwani,ambapo madiwani hao walipendekeza maeneo ya kuhamia wamachinga hao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Musa Mapunda,alipotakiwa kutaja kiongozi aliyeamuru mgambo hao kuendesha oparesheni ya kuwatoa machinga wakati mazungumzo yalikuwa mezani kati ya viongozi wa wafanyabiashara hao,alisema mgambo hao hawakutumwa bali walikuwa kwenye utekelezaji wa kawaida wa majukumu yao .

No comments: