Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, November 8, 2011

MKUU WA MKOA WA MBEYA ABAS KANDORO AUPOKEA MWENGE WA UHURU

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya (kulia), akimkabidhi mwenge
wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro,baada ya mwenge huo
kumaliza mbio zake mkoani Rukwa, katika hafla iliyofanyika jana, kijiji
cha Mkutano wilayani Mbozi.
Askari wa kutuliza ghasia na skauti wakiulinda mwenge wa uhuru baada ya kuwasili viwanja vya Bomani wilayani Mbozi.
Mkimbiza
Mwenge Kitaifa,Mtumwa Rashid Halfan, kutoka kaskazini Unguja, akivuta
pazia kuashiria uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa Kiume wa Sekondari ya
Mwalimu Jk.Nyerere iliyopo Tunduma wilayani Mbozi mkoani Mbeya.
Wakimbiza
Mwenge kitaifa wakisikiliza wimbo wa kupinga Rushwa uliokuwa ukiimbwa
na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ihanda iliyopo Mozi wakati wa
uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa shuleni hapo.
Wananchi
wa Mkoa wa Mbeya wakishangilia baada ya mwenge wa uhuru kuwasili
katika kijiji cha mkutano ambacho kipo mpakani mwa mkoa wa Rukwa na
Mbeya.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo (kulia), akimkabidhi mwenge wa Uhuru
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini,Evance Balama, baada ya mwenge huo
kumaliza mbio zake wil;ayani Mbozi.Makabidhiano hayo yalifanyika Songwe
Viwandani mkoani Mbeya.Mwenge huo mkaoni Mbeya utafungua miradi yenye
thamani ya sh.bilioni 2.6 na Wilayani Mbozi umefungua miradi mitatu ya
sh.milioni 156. 

(PICHA ZOTE NA DOTTO MWAIBALE)

No comments: