Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, November 11, 2011

MBEYA CITY NA PRISONS ZAPEWA PONGEZI BAADA YA KUFANYA VIZURI KATIKA LIGI DARAJA LA KWANZA.

Na Joachim Nyambo,Mbeya.
Wadau wa mchezo wa mpira wa miguu mkoani hapa wamezipa pongezi timu za Mbeya City na Tanzania Prisons zinazoshiriki ligi daraja la kwanza katika kundi B kwa kufanya vizuri katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo uliomalizika hivi karibuni.

Pamoja na pongezi hizo,wadau hao wametoa sababu iliyoonekana kuwa chanzo cha Tanzania prisons kutofanya vizuri katika michezo yake ya kwanza ya mzunguko huo lakini kadiri ilivyoendelea ikaonekana kuanza kufanya vizuri na hatimaye kumaliza mzunguko huo ikiwa na jumla ya pointi tano na magoli mawili ya kufunga.

Makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoani hapa MREFA Ben Mwamwaja ni miongoni mwa wadau walizungumzia hali hiyo ambapo alisema kocha wa timu hiyo Steven Makata kutokaa muda mrefu na timu kulisababisha akose kikosi alichokiamini na kulazimika kupanga kikosi kipya kila mchezo.

Mwamwaja alisema hali hiyo iliwasababishia wachezaji kutoelewana uwanjani na kujikuta ikipoteza mchezo husika hata ilipocheza na timu zisizo na uwezo wa kuifunga zilizomo katika kundi B hilo.

Mdau mwingine Amosi Chuma alisema mafanikio yaliyoonyeshwa na Tanzania prisons katika michezo yake ya mwisho ya mzunguko huo yanaleta matumaini kuwa tayari kocha Makata alipata kikosi kilicho na uwezo hivyo upo uwezekano mkubwa wa timu hiyo kufanya vyema katika mzunguko wa pili utakaoanza January mwakani.

“Unajua awali ilionekana kocha haamini kabisa wachezaji wake.Ndiyo sababu kila mchezo ikaonekana anachezesha wachezaji wapya sasa ile ilikuwa ngumu kwa timu kuelewana na kufanya vizuri.Lakini mwishoni tuliona kikosi chake kinaanza kutulia na kufanya vizuri.Sasa tunaamini kuwa mzunguko ujao Prison nayo itafanya vizuri” alisema Chuma.

Katika mzunguko huo wa kwanza Tanzania prison ilianza vibaya kwa kufungwa goli 1-0 na ndugu zao timu ya jiji la Mbeya,ikatoka suluhu ya bila kufungana katika michezo miwili iliyocheza na Small Kids ya Rukwa pamoja na PolisiIringa,ikafungwa goli moja bila na JKT Mlale na mwishoni ikazinduka na kuifunga Majimaji ya Songea goli 2-1.

Kwa upande wa timu ya jiji Mbeya City inayoongoza katika kundi hilo ikiwa na jumla ya pointi 13,baada ya kuifunga Tanzania Prisons,iliifunga JKT Mlale goli 3-1 kabla ya kutoka suluhu ya goli 1-1 na Majimaji,Ikaifunga Polisi Iringa 1-0 na mchezo wa mwisho ikainyuka Small Kids 4-1.

No comments: