Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 2, 2011

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YAPIGA MARUFUKU UPANGAJI BIDHAA NJE YA MADUKA

Mkurugenzi wa jiji la mbeya Juma Iddi kushoto akionge na waandishi wa habari Chales Mwakipesile Majira  Osea Cheo TBC na Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu

Mkurugenzi huyo wa jiji la mbeya amesema ni marufuku kuweka bidhaa nje ya maduka kwani imekuwa ni kero kwa waenda kwa miguu na usafi wa jiji kwa ujumla maana bidhaa zao hupanga mpaka barabarani hivyo kuwakosesha waenda kwa miguu eneneo la kupita
hivyo kuanzi sasa kila mfanyabiashara jijini mbeya aweke bidhaa zake ndani ya duka lake atakaekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali na kulipa faini ya sh 50,000/
Baadhi ya maduka yaliyopanga bidhaa zao nje ya maduka ambayo sasa utaratibu huo umepigwa marufuku na jiji la mbeya

2 comments:

Kelkaf said...

Kweli huu ni unyanyasaji kwa wafanyabiashara...kwanza watu wengi hufanya usafi wenyewe kwenye maeneo yao ya kazi na kweli maeneo mengi ya maduka yamekuwa mstari wa mbele katika swala la usafi bila msaada wa wasafisha jiji, na pili hiyo kero ya waenda kwa miguu ndo kwanza naisikia kwa huyu mkurugenzi utadhani yeye ndo anapita pita kwenye maeneo ya biashara ya watu...kweli sijui tutafika wapi na unyanyasaji huu walianza kwa wamachinga sasa wamefika mpaka hapa

zitto kiaratu said...

wamekosa ulaji hao wanatafuta cha kutia mfukoni, wakubwa wanakula nchi sasa tusishangae vijigogo kama hawa!!!!!