Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, October 23, 2011

WAZIRI MEMBE ATEMBELEA BANDA LA WAJASIRIAMALI WANAODHAMINIWA NA UN WAKATI MAADHIMISHO YA WIZARA YAKE YA MIAKA 50 YA UHURU.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akinusa bidhaa ya mshumaa inayotengenezwa na wajasiriamali wanaodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa wakati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilipofanya maadhimisho ya kusheherekea miaka 50 ya Uhuru jijini Dar es Salaam.Wa kwanza Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa J&L Handicrafts Louise Judicate Mushi na Katikati ni Mwakilishi UN Communication Group (UNCG) Magnus Michael Minja.
Waziri Membe akichagua moja ya mashati katika banda hilo.
Waziri Membe akikagua bidhaa kwenye banda la Mama Magessa Muna kutoka Kym's Enterprises.
Waziri Membe akikagua zulia lililotengenezwa kwa ngozi ya mnyama katika banda la Famour Designer. Anayetoa maelezo kwa Waziri ni Fashion Designer Fatma Amour.
Waziri Membe akifafanua jambo.
Bi.Fatma Amour akionyesha zulia lililotengenezwa kwa ngozi ya Mbuzi kwa Mhe. Mgeni rasmi Waziri Membe.
Mheshimiwa Mgeni rasmi akipata ufafanuzi kutoka kwa Youth Coordinator Mussa Haji alipotembelea katika Banda la Umoja wa Mataifa la Youth of United Nations Associations of Tanzania.
Waziri Membe akipewa makabrasha mbalimbali.
Mgeni rasmi Mhe. Membe akizungumza na Programme Officer wa UNAIDS Amandine Oleffe katika banda la UNAIDS.
"Thanks you for Visiting and Welcome Again".

(Picha kwa hisani ya www.mohammeddewji.com/blog)

No comments: