Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, October 25, 2011

WATENDAJI WA HALMASHAURI NA WILAYA WAMETAKIWA KUONDOA URASIMU WA TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI MBEYA.

Katibu Tawala msaidizi Utumishi na utawala Bwana Leoonard Magacha akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya 
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club Christopher Nyanyembe akisisitiza ushirikiano  kati ya ofisi ya mkuu wa mkoa Mbeya na wanahabari katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa mbeya

Waandishi wa habari wakongwe na waliobobea mkoani Mbeya wakimsikiliza katibu tawala msaidizi bwana Magacha
*****
Na mwandishi wetu
Katibu tawala msaidizi Utumishi na Utawala Bwana Leonald Magacha amewataka watendaji wa halmashauri na wilaya kuondoa urasimu wa taarifa kwa waandishi wa habari ili kuiwezesha jamii kutambua mambo yanayoendelea katika mkoa wao.


Ameyasema hayo kufuatia kuwepo kwa tabia ya baadhi ya wakuu wa idara kutoka halmashauri mbalimbali kutokuwa na ushirikiano na vyombo vya habari katika kutoa taarifa hali inayowalazimu waandishi wa habari kutafuta njia mbadala ya kupata habari hizo.

Naye mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Christopher Nyenyembe ameuomba uongozi wa Serikali mkoani hapa kuondoa ubaguzi wa vyombo vya habari katika kutoa taarifa ili kuondoa hisia binafsi za mtu katika utendaji kazi.

No comments: