Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, October 5, 2011

SERIKALI YAOMBWA KUPANGA BEI MAALUMU YA ZAO LA KOKOA WANANCHI+KYELA+MBEYA

 
Na mwandishi wetu.
Wakulima wa zao la Kakao wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wameiomba serikali kutoa msimamo wa bei ya uuzaji wa zao hilo ili kumwezesha mkulima kunufaika na kilimo hicho.

Ombi hilo limetolewa na mkazi wa kijiji cha Matema wilayani humo Bwana Peter Humbo ambaye anamiliki shamba la zao la Kakao lenye ukubwa wa hekta 4 zenye uwezo wa kutoa Tani 2 za zao hilo kwa msimu mmoja.

Amesema bei ya kakao kwa hivi sasa imepanda kutoka shilingi elfu moja mia sita hadi kufikia shilingi elfu mbili mia nne kwa kilo moja.

Hata hivyo amesema kushuka na kupanda kwa bei ya zao hilo ni changamoto kwa wakulima kujitayarisha na msimu mwingine wa kilimo kutokana na kupanda kwa ghalama za pembejeo za kilimo.

Pamoja na hayo wameiomba serikali kuongeza mawakala wa ununuzi wa zao hilo ili kuleta ushindani katika biashara  na kuleta mafanikio kwa mkulima.

Amewata makala wanaonunua zao hilo kwa sasa kuwa ni Kampuni ya Mohammed Interprises Ltd na Biolends Interprises Ltd  ambayo makao makuu yake ni mkoani hapa.

No comments: