Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, October 29, 2011

RADI YASABABISHA KIFO NA KUJERUHI - MBEYA.

Na mwandishi wetu
Bi Magdalena Mlaga mwenye umri wa miaka 28 amefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya kupingwa na radi akiwa ndani ya nyumba yake, radi hiyo ambayo ilisababishwa na mvua iliyokuwa ikinyesha juzi katika kijiji cha Iyenga, kata ya Isansa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

Chanzo chetu kutoka eneo la tukio kimeeleza kuwa mvua hiyo ilianza kunyeesha majira ya saa saba za mchana na ilimalizima majira ya saa nane unusu mchanaambapo marehemu akiwa na mwanae Happy Mwakanyonga mwenye umri wa miaka mitatu pamoja na mdogo wake Gift Yona mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Mpito walipingwa na radi hiyo.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo bwana Efraimu Mwampanda amesema kuwa baada ya tukio hilo kutokea walimkuta Bi.Madawa Malaga akiwa amelala na ndipo walipomfikisha hospitali ya Vwawa Mbozi na kuambiwa kuwa amefariki dunia na kwamba mdogo wake aliendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Hata hiyo Mtoto Happy Mwakanyonga hakukutwa na tatizo lolote.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletusi Malindisa amesema kuwa hana taarifa ya tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi baada ya kulifuatilia.

No comments: