Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, October 25, 2011

MTU MMOJA AFARIKI KWA KUJINYONGA MTAA WA MWAMBENJA - KATA YA IGANZO MKOANI MBEYA. Mtu mmoja mkazi wa mtaa wa Mwambenja kata ya Iganzo jijini Mbeya aliyefahamika kwa jina la Anyimike Ambokile mwenye umri wa miaka 25, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya plastiki chumbani kwake, na hakuacha ujumbwe wowote wa kukatiza maisha yake. Marehemu alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza mitumba katika soko la Sido Mwanjelwa lililoteketea kwa moto hivi karibuni.(Picha juu ni sehemu ambayo marehemu alijinyonga)
Kifo cha Anyimike Ambokile kiligunduliwa na mama wa marehemu aitwaye Esther Tujobe mwenye umri wa miaka 60, wakati akijiiandaa kuelekea kanisani ndipo agagundua marehemu hajaamka mapema kwenda kwenye shughuli za kuuza mitumba na kukuta mwanae akiwa amefariki na hivyo kulazimika kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa wa Mwambenja Bwana Lucas Mwakalonge ambaye nae alitoa taarifa kwa Diwani wa kata ya Iganzo Bwana Uswege Furika ambaye alitoa taarifa kwa Kituo cha Polisi cha Kati jijini Mbeya ambapo walifika na kuuchukua mwili wa marehemu  hadi Hospitali ya RufaaMkoani Mbeya kwa uchunguzi zaidi ambapo jalada lake ni MB/IR/9204/2011

No comments: