Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, October 23, 2011

MKUU WA MKOA MBEYA AWATAKA WAZEE NA MACHIFU MKOANI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUDHIBITI VITENDO VYA UHALIFUMkuu wa mkoa wa Mbeya mheshimiwa Abas Kandoro
*****
Na mwandishi wetu
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amewataka wazee na machifu mkoani hapa kushirikiana na Serikali katika kudhibiti vitendo vya uhalifu pamoja na kurejesha maadili ya mtanzania ambayo yameaza kumomonyoka kutokana na utandawazi.

Agizo hilo amelitoa katika mkutano kati yake na wazee maarufu na machifu mkoani hapa kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mkapa na kuhudhuriwa na viongozi wa kimila zaidi ya 70.

Kandoro amesema Ubinafsi, Kupungua kwa uzalendo wa taifa, Uhuru usio na mipaka na kukua kwa utandawazi kumechangia kwa kiasi kikubwa jamii kupotoka kimaadili hali ambayo inahitaji busara na hekima kutoka kwa wazee ili kuirejesha.

Naye mwenyekiti wa umoja wa wanajamii Tanzania (MUJATA) bwana Shayo Masoko ameahidi kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kurejesha nidhamu ya kazi na utendaji kazi kwa kuzingatia sheria ili kuifanya jamii kuwa salama.

No comments: