Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 28, 2011

Mkutano wa CHOGM 2011 wafunguliwa leo Mjini Perth,Australia

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (watatu kulia mstari wa pili) akimsikiliza Malkia Elizabeth II wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuia ya madola leo mjini Perth nchini Australia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (watatu kulia mstari wa pili) akiwa na baadhi ya wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya madola wakimsikiliza mtu mwenye asili ya watu wa Australia ( anaeonekana kwenye king'amuzi) akielezea asili ya nchi hiyo leo mjini Perth nchini Australia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuia ya madola.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete wakikaribishwa na Aaron Verlin (kulia) ambaye ni Meneja wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuai ya Madola kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo Perth Nchini Australia. Malkia Elizabeth II wa Nchini Uingereza ndiye aliyefungua mkutano huo.
Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.

No comments: