Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, October 20, 2011

MJASIRIAMALI AIOMBA SERIKALI KUFUNGUA MADUKA YA KUUZA VIFAA VYA USINDIKAJI - MBEYA

Maboga tayari kwa biashara sokoni.
*****
Na mwandishi wetu
Serikali imeombwa kufungua maduka ya kuuza vifaa vya usindikaji mkoani Mbeya ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kupata vifaa kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

Ombi hilo limetolewa na Bi.Sarah Mtalemwa ambaye anajihusisha na shughuli za usindikaji na utengenezaji wa waini ya Twinsi amesema kupitia kazi hiyo ya usindikaji wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la upatikanaji wa vifaa vya kusindikia kutokana na vifaa hivyo kupatikana Dar es salaam pekee.

Ameongeza kuwa ili kurahisisha kazi za ujasiriamali ziweze kufanyika kwa urahisi na kuwawezesha wao kupata kipato kutokana na shughuli zao za usindikaji.

Twinsi waini hutengenezwa kwa kutumia maboga na Losera ambapo chupa moja ya waini yenye ujazo milizi 750 huuzwa kwa shilingi 5,000 na yenye ujazo wa milizi 250 huuzwa kwa shilingi 2,500.

No comments: