Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, October 27, 2011

MBUNGE MBEYA ASEMA HATOKIHAMA CHAMA CHA MAPINDUZI

Mbunge wa jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi(katikati), akisalimiana na baadhi ya wananchi nje ya mahakama ya Hakimu mfawidhi wa mkoa wa Mbeya.
*****
Na mwandishi wetu.
Mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Modestus Kilufi kupitia chama cha Mapinduzi amesema kuwa hana mpango wa kukihama chama cha Mapinduzi (CCM) licha ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizosababishwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho.

Ameyasema nje ya Mahakama ya mkoa wa Mbeya mara baada ya kutoka mahakamani hapo kutoa utetezi wake dhidi ya kesi inayomkabili ya kutishia kuuwa.
Amesisitiza kwamba changamoto zilizopo kati yake na wanachama wenzake wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbarali haiwezi kumvunja moyo wa kuwatetea wananchi bali ni njia ya kumwongezea nguvu katika kusimamia masuala muhimu yanayowakabili wananchi wa jimbo lake.

Wakati huohuo ameitaka jamii kutambua kuwa utetezi wa wananchi haufanywi na chama fulani cha siasa bali ni jukumu la kila kiongozi kuwatumikia wananchi wake kuwatetea kwa uongozi wa juu ili kero zao ziweze kutatuliwa.

Hukumu ya Mbunge huyo itatolewa Novemba 9 mwaka huu baada ya pande zote za ushahidi kumaliza kutoa ushahidi wao.

No comments: