=====
Na mwandishi wetu.
Baadhi ya wachungaji wa kanisa la kiijili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya Konde wamesema hawana imani na kamati ya utekelezaji wa halmashauri ya kichungaji inayoongozwa na Baba askofu Dakta Peter Mwakyolile ambayo inasimamia maadili na usuluhishi baina ya wachungaji.
Wakizungumza na chanzo hiki kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutotajwa majina yao wachungaji hao wamesema kujiuzulu kwa Katibu wa kamati hiyo Mchungaji Michael Ambangile kumetokana na mvutano wa muda mrefu kati yake na mkuu wa Jimbo la Magharibi Mchungaji Nyibuko Mwambola ambaye ni mjumbe wa kamati.
''Sababu ya kujiuzulu kwangu ni kutokana na mvutano wa muda mrefu kati yangu na mtumishi mwenzangu'' alisema Mchungaji Ambangile kupitia barua iliyomwandikia Askofu wa dayosisi hiyo.
Nao baadhi ya wachungaji na waumini wamemwomba Askofu wa dayosisi hiyo kuivunja kamati iliyoteuliwakwani baadhi ya wajumbe huendekeza majungu, mabishano na malumbano yasiyokuwa na tija yoyote kwa kanisa.
Kwa upande wake Mwambola amesema hajawahi kuwa na ugomvi na Mchungaji Ambangile na hajapata nakala ya barua iliyoandikwa kuhusu malalamiko yanayomkabili.
No comments:
Post a Comment