Na mwandishi wetu.
Serikali na imeitaka jamii kujishughulisha katika shughuli zilizo halali ambazo zinawawezesha kujipatia kipato badala ya kujishughulisha katika vitendo haramu ambavyo vimekuwa vikiwapelekea baadhi yao kuingia mikonono mwa sheria na wengine kuishia mikononi mwa wananchi wenye hasira kali.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evansi Balama kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi katika kampeni za kushawishi jamii kutii sheria bila kushurutisha kwa lengo la kudumisha amani, usalama na utulivu mkoani hapa.
Amesema uwajibikaji katika kazi ndio njia pekee itakayo mwezesha mwananchi kujipatia kipato na sio kwa njia ya unyang'anyi na kujiingiza katika shughuli haramu.
Awali akimkaribisha Mkuu wa wilaya, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa kupitia kampeni hiyo Jeshi la polisi linatarajia kuona ushirikiano bora kati yao na wananchi katika kusimamia ulinzi wa mali na maisha ya raia.
No comments:
Post a Comment