Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, October 12, 2011

26 WAKAMATWA KWA UHALIFU WA UPIGAJI NONDO MKOANI MBEYA

Bwana Elia Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakijiuguza majeraha katika Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1 baada ya kupigwa nondo hivi karibuni.
*****

Na mwandishi wetu
Watu 26 wamekamatwa kwa kuhusika na matukio ya upigaji Nondo mkoani Mbeya ambapo watuhumiwa wamegawanyika katika makundi matatu huku kila kundi likiwa na watu 4 hadi 15.

Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ameyataja makundi hayo kuwa kundi la kwanza linawahusisha watu wanne ambao ni Herodi Luka, Musa Idi, Fadhili Luvanda na David Jimy waliosababisha vifo vya watu wawili.

Kundi la pili linawatu saba ambao ni Edson Ulendo, Rashidi Mwakyungwe, Elasto Eliasi, Musa Isa, Amosi Mziho, Sifa Jolewa na Frenk Kitonga ambao walisababisha kifo cha Pc Meshaki

Kundi la mwisho linawahusisha watu 15 ambao wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na kwamba kundi la kwanza na la pili yamekubali kuhusika na matukio ya upigaji nondo.

Wakati huohuo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ametoa shukrani kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa matukio ya upigaji nondo na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kudhibiti vitendo vya uhalifu.

No comments: