Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, September 7, 2011

WAUMINI WA MADHAHEBU MBALIMBALI MKOANI MBEYA WAMETAKIWA KUTOKATA TAMAA KIMAISHA KUTOKANA NA MAISHA MAGUMU.


Waumini wakizama kwa maombi.
Na mwandishi wetu.
Waumini wa madhehebu mbalimbali mkoani Mbeya wamehamasishwa kutokata tamaa wakati wa kukabiliana na changamoto wanazokabiliwa katika maisha ya kila sikun ndani ya jamii.

Akihubiri katika Usharika wa Sinai Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli (KKKT) Dayosisi ya Konde Bi.Marium Kyomo alisema wananchi wanapaswa kupambana na kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo kama vile za kiuchumi na kwamba wanapaswa kujiunga katika jumuiya moja na kutatua kwa njia zilizo sahihi na kwamba kukimbia sio suluhisho.

Aidha ameongeza kuwa kukata tamaa maishani huleta hofu mashaka na kutojithamini hali inayoweza kusababisha mtu kuhisi kama hapendwi na Mungu.

Hata hivyo amesisitiza kuwa katika kukabiliana na changamoto za maisha ni vyema kutumia ufumbuzi usiokwenda kinyume na mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwani Muumba huwaadhibu wanaokaidi amri zake.

No comments: