Na mwandishi wetu.
Afisa mtendaji wa kata ya Itezi jijini Mbeya Bwana Gwakisa Angetile amewataka wakazi wa kata hiyo kushirikiana katika ulinzi ili kuwafichua wahalifu.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu katika kata hiyo hali inayosababisha hofu ya usalama wa maisha na mali zao.
Aidha Bwana Angetile amesema kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikijitokeza hasa nyakati za usiku jambo ambalo linalopelekea uongozi wa kata hiyo kuwataka kushirikiana ili kulinda usalama wa mali zao
No comments:
Post a Comment