Na mwandishi wetu.
Wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga jijini Mbeya wamelalamikia tamko la halmashauri ya jiji kuwataka kuondoka katika maeneo wanayofanyia biashara pasipo kuwaonesha sehemu nyingine.
Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya wafanyabiashara hao Bwana Baraka Daudi na Bwana Nicholous Msingwa wamesema kuwa halmashauri hiyo haijawashirikisha katika maamuzi waliyoyatoa japokuwa wamefanya uamuzi mzuri lakini wanaomba watengewe eneo kwa ajili ya kuendeshashughuli zao.
Aidha wafanyabiashara hao wanaiomba serikali iwape muda wakuendeleza biashara zao hadi pale watakapotengewa eneo lao ili kuendelea na biashara zao.
Wameongeza kuwa kutengewa eneo maalumu itatoa mchango mkubwa kwao kufanyabiashara kwa uhuru na kwa matumaini ili kuweza kujiongezea kipato na kwamba kutangatanga itachangia kuyumba kiuchumi kwa wengi wao wanategemea biashara hiyo katika kuendesha familia zao.
Hata hivyo wamekuwa wakiendesha biashara zao kwa kuchukua mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha ikiwa ni pamoja na Pride, Saccos, hivyo kuhamishwa huko kwa ghafla kutawaathiri katika urudishaji wa mikopo hiyo.
Wamehitimisha kwa kusema utaratibu wao wakibiashara hutegemea kuwakopesha wateja wao hivyo kuwapata sehemu wanazohamishiwa itakuwa vigumu na matokeo yake ni wanahesabu wamepata hasara.
No comments:
Post a Comment