Imeelezwa kuwa wafanyabiashara wa eneo hilo wamekuwa wakitumia udhaifu wa jamii ya wasukuma kutojua kusoma na kuandika kuwatisha kwa kuwatumia askari polisi wachache wasiotimiza vyema wajibu wao pamoja na mahakama ambapo katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa zaidi ya wafanyabiashara hao hufanya ujanja huo wakati wa msimu wa mavuno ya zao la mpunga au msimu ya kuuza mifugo.
Katika hali ya kutumia vibaya vyombo vya sheria na dola(mahakama na polisi), mwananchi mmoja wa kijiji cha Lwanjili kata ya Chimala amejikuta akikamatwa na kufungwa pingu kwa kile kinachodaiwa kuwa alikopa shilingi 160,000/= kutoka kwa mfanyabiashara Bwana Khamis Mwangela maarufu kwa jina la Khamis Kichwa.
Tukio hili limetokea Septemba 12, mwaka huu ambapo Bwana Kulwa Machagunya alikamatwa na kupelekwa katika mahakama ya mwaanzo ya Chimala bila kujua kosa lake huku akisindikizwa na ulinzi mkali wa Polisikutoka kituo cha Chimala.
Baada ya kufikishwa mahakamani kutokana na barua ya wito iliyoandikwa na mahakama hiyo iliyokuwa na Kumbukumbu namba MADAI CH/PR/KUMB/30/2011 mahakama ilishindwa kumsomea shitaka hivyo hakimu akatoa kipeperushi kilichomwagiza Mkuu wa kituo cha Chimalakumfungulia mashtaka Bwana Kulwa Machagunya kuwa alikopeshwa fedha yenye thamani ya shilingi 160,000/= za kitanzania na Bwana Khamis KIchwa mapema mwezi Februari kitu ambacho si kweli.
Hatua hiyo iliyopelekea Mkuu wa kituo hicho kukataa agizo hilo la Hakimu wa mahakama hiyo na kumwachia huru mshitakiwa kwa damana iliyotolewa na ndugu zake.
Hata hivyo imedaiwa kuwa mfanyabiashara Khamis amekuwa akiwasiliana na Hakimu kwa simu kwa mara nyingne kumtumia kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mwinuka na hatimaye kijana huyo kushindwa kuthibitisha madai hayo mbele ya mkuu wa kituo.
Baada ya kutofika kituoni mlalamikaji mkuu wa kituo hicho aliamua kuwa Khamis na Kurwa wafike kituoni siku ya Jumamosi majira ya saa mbili asubuhi.
Kwa mujibu wa diwani wa kata ya Chimala Bwana Hussein Wahaya "Swali linakuja kama Khamis ni mkiopeshaji wa pesa mbona asasi kama benki himtambui kama benki au taasisi ya kuweka na kukopa SACCOS na kwamba kama yeye ni mkopeshaji mbona hakuna mkataba wowote baina ya mkopeshaji na mkopaji?"
No comments:
Post a Comment