Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, September 3, 2011

TANZANIA KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU IKIWA NA MAKUNDI YA WATU MAKABWELA NA WENYE NACHO!




David Kafulila (Katikati)

Tanzania inaenda
kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wakati uchumi wake ukikabiliwa na tofauti
kubwa ya kimapato baina ya kundi la Watanzania makabwela na lile la
walio nacho ambao wamekuwa wakiishi kwa kukata tamaa kutokana na
matabaka hayo.

Akizungumza kwenye mkutano
wa hadhara kuelekea miaka 50 ya Uhuru kwenye viwanja vya Temeke Jijini
DSM Mbunge wa Kigoma Kusini DAVID KAFULILA amesema uchumi wa kundi la
walionacho ambao ni Mawaziri, Wabunge, Maktibu Wakuu na Wafanyabiashara
wakubwa unakuwa wakati ule wa makabwela ukiporomoka zaidi.

Kutokana na hilo
Mheshimiwa KAFULILA ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa NCCR – Mageuzi
ametoa wito kwa serikali kufikiria upya uamuzi wa kujiunga kwenye soko
la pamoja la Afrika Mashariki ili kuepuka wananchi kuishia kuwa vibarua.


No comments: