Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, September 22, 2011

NJAA NI CHANZO CHA WANAFUNZI KUFELI KATIKA UTAFITI WA AFISA ELIMU MKOA WA MBEYA. BWANA JUMA KAPONDA

Na mwandishi wetu.
Afisa elimu mkoa wa Mbeya Bwa Juma Kaponda amesema utafiti wa awali umeonesha kuwa wanafunzi wa shule za msingi wamekuwa wakifeli mitihani yao kutokana na kusoma wakiwa na njaa hivyo kushindwa kuelewa wafundishwapo wawapo darasani.

Wakati huohuo amewataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kutoanguvu kazi na michango itakayowezesha ukarabati wa shule pindi madarasa yanapoharibika ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.

Awali wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi, eneo la Mlima reli walise,a watashiriki kuchangia chakula kwa wazazi wanaosoma katika shule ya Msingi Mlima reli, endapo serikali itaboresha miundombinu ya shule hiyo.

Wakiongea na mwandishi wetu wamesema itakuwa jambo la aibu kwa wanafunzi kuboreshewa chakula wakati wakisoma katika madarasa mabovu huku shule ikiwa haina huduma ya maji safi na salama.

No comments: