Na mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana John Livingstone Mwakipesile amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe Bwana Noel Mahenga kuwafikisha katika vyombo vya sheria watumishi wa serikali waliohusika na kashfa ya kuwatoza faini ya shilingi 500 na kutowapa stakabadhi wananchi wanaodaiwa kutokuwa na vyoo pamoja na mazingira machafu ya nyumba zao.
Watumishi hao walichukua hatua hiyo walipokwenda kufanya operasheni ya usafi wa mazingira vikiwemo vyoo katika kata hiyo,hata hivyo badala ya kutekeleza kilichowapeleka waligeuza kama mbinu ya kujipatia fedha na mazao ya wakulima walioshindwa kulipa fedha hiyo.
Naye mmoja wa wananchi hao Philipo Mwakatumbula alisema kitendo kinachofanywa na idara hiyo ni kibaya kwani wanateseka kwa kushindwa kulipa shilingi mia tano na kunyang’anywa mazao yao ambayo wanategemea kwa chakula na kujipatia fedha.

No comments:
Post a Comment