Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, September 3, 2011

Mgombea Ubunge Jimbo La Igunga-CCM Dk. Dalally Kafumu Achukua Fomu


MKURUGENZI wa Uchaguzi jimbo la Igunga Magayane Protace (kulia) akimkabidhi fomu za kuwania ubunge wa jimbo hilo, mgombea mteule wa CCM Dk. Dalally Kafumu , jana. Wengine ni Katibu wa CCM wilaya ya Igunga Neema Adamu na Msimamizi wa masuala ya uchaguzi wa CCM, Matson Chiz
MGOMBEA mteule wa CCM jimbo la Igunga Dk. Dalally Kafumu (kushoto) na Mratibu wa Uchaguzi wa CCM jimboni humo, Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba wakiwa katika huzuni kwenye hospitali ya wilaya ya Igunga ambako walisaidia kupeleka mwili wa mtoto Peter Ezekiel ambaye alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo katika barabara ya Igunga-Singida akijarbu kuvuka barabara akiwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo waliokuwa wakimsubiri Kafumu na msafara wake, jana. Kulia ni ndugu wa mtoto huo.
MGOMBEA mteule wa CCM jimbo la Igunga Dk. Dalally Kafumu (kushoto) na Mratibu wa Uchaguzi wa CCM jimboni humo, Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba wakimfariji Kulwa Mpina baada ya kufikisha kwenye chumba cha kuhifadhi maiti mwili wa mtoto Peter Ezekiel ambaye alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo katika barabara ya Igunga-Singida akijarbu kuvuka barabara akiwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo waliokuwa wakimsubiri Kafumu na msafara wake, jana.
Picha na Bashir Nkoromo





No comments: