Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe (kulia) akionyesha ishara ya kumwombea kura mgombea udiwani kata ya Gangilonga jimbo la Iringa mjini Edwin Sambala wakati akijinadi kwa wananchi leo
Mbowe akiwaaga wananchi wa kata ya Gangilonga baada ya kumaliza kumwombea kura mgombea wa kata ya Gangilonga na Kitanzini jimbo la Iringa mjini.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao akiwaombea kura wagombea udiwani wa Chadema kata ya Gangilonga na Kitanzini leo
Mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga Edwin Sambala akimsikiliza mwenyekiti wake taifa Mhe.Mbowe
Mgombea udiwani kata ya Kitanzini Gervas Kalolo
Wananchi wa kata ya Gangilonga na Kitanzani waliofika katika mkutano wa Chadema kata ya Gangilonga wakigombea kumsalimia Mbowe jana
Diwani wa CCM kata ya Mgama Denis Lupala (kulia) akisalimiana na makada wenzake waliofika katika mkutano wa Chadema leo,
Wana Chadema wakisalimiana na Mbowe
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Mhe.Mbowe akiondoka Iringa baada ya kumaliza mikutano ya kampeni ya Chadema
Gari la Mbowe likisindikizwa na mashabi eneo la Kitanzini leo
Umati wa wananchi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake ukiwa katika kata ya Gangilonga kumsikiliza mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe.Mbowe wakati akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Kitanzini Gervas kalolo
Wananchi wa kata ya kitanzini na kata mbali mbali za manispaa ya Iringa wakiwa katika mkutano wa Chadema leo
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe.Mbowe kati kati na mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akiwa na katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Susana Mgonakulima
Wananchi kiduchu wa kata ya Gangilonga wakimsikiliza Mbowe jana
Wadau wa mziki pia wakimsikiliza Mbowe na MR.Sugu leo
MWENYEKITI wa Taifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe awataka wananchi wa kata ya Gangilonga na Miyomboni Kitanzini katika jimbo la Iringa mjini kutotishwa na viongozi wa serikali na badala yake kuchagua madiwani wa Chadema ili kuwatumikia vema wananchi badala ya madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) ambao wapo kwa ajili ya kuwakilisha mafisadi.
Na Francis Godwin
Mbowe alitoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Gangilonga katika jimbo la Iringa mjini ambapo alisema kuwa hajapendezwa na hatua ya serikali ya CCM kutoa vitisho kwa wananchi wa eneo hilo ambao watashiriki mkutano huo wa kampeni .
Mbowe pia aliwataka wananchi Gangilonga kumpa kura Edwin Sambala huku wale wa Kitanzini kumchagua Gervas Kalolo na si mwingine.
Alisema kuwa idadi ndogo ya wananchi waliofika katika viwanja hivyo vya mkutano ni kielelezo tosha kuwa wananchi wa kata hiyo wametishwa kushiriki katika mkutano huo japo alisema kuwa haisaidii kwani hata kama CCM itatumia vitisho kuzuia watu kusikiliza mikutano ya kampeni ila bado hukumu ipo pale pale siku ya uchaguzi ambapo kila mwananchi atatumia haki yake ya kidemkrasia kumchagua kiongozi bila vitisho.
Hata hivyo alisema kuwa aliwataka wananchi wa Gangilonga na Kitanzini na kata nyingine zote ambazo zina uchaguzi mdogo wa madiwani kuungana na wananchi wa jimbo la Igunga kwa kukitosha chama cha CCM na kuchagua viongozi wa Chadema ambao wapo kwa ajili ya maslahi ya watanzania .
Alisema kuwa ushahidi wa utendaji kazi wa viongozi wa Chadema umejionyesha katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambako Chadema ina uwakilishi wa wabunge 48 ila ndio ambao wanaonyesha kuwajibika vema kuliko wabunge zakidi ya 200 wa CCM ambao wameendelea kulala bungeni.
Mbowe alisema kuwa serikali ya CCM imeendelea kufanya ufisadi mkubwa wa raslimali za Taifa hili ila watanzania wachache wameendelea kuikumbatia na kuwa sasa Mungu ameaamua kuikomboa Tanzania kwa kuifanya Chadema kuwa chama cha ukombozi wa watanzania.
“Tunasema kuwa Chadema hatuogope polisi tunawaheshimu na ifikapo mwaka 2015 lazima ikulu iwe chnini ya Chadema na CCM imefika wakati wa kupumzishwa na kuwa maandalizi hayo yanapaswa kuanzwa kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga na udiwani katika kata zote”
Mbowe alisema kuwa Tanzania inaweza kuendelea bila Rais kutoka ndani kwenda Marekani kuomba vyandarua wala kwenda kuomba misaada mbali mbali na kuwa Taifa linadhalilishwa na Ikulu kwa kuendekeza omba omba kwa nchi mbali mbali
Katika hatua nyingine Mbowe alieleza kusikitishwa na misafara mikubwa ya viongozi wa serikali na ziara za mara kwa mara nje ya nchi kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Hata hivyo asema ni aibu kwa Rais kuendelea kutembeza bakuli nje ya nchi huku Taifa lina uchumi mkubwa wa madini ambao umeshindwa kusimamiwa vema
Kuhusu kupigwa kwa mkuu wa wilaya ya Igunga na mashabiki wa Chadema Mbowe alisema kuwa kipigo alichokipata na haki yake na kuwa wapo tayari kumshughulikia hata kama mkuu wa mkoa iwapo atataka kuchakachua matokeo ya ushindi wa Chadema Igunga
Alisema kuwa kati kata zote zaidi ya 20 zinazogombea katika uchaguzi mdogo wa udiwani CCM itegemee kuchukua kata 4 pekee na katika jimbo la Igunga CCM itegemee kushika nafasi ya mwisho katika uchaguzi huo ambapo jimbo hilo hadi sasa tayari ushindi upo kwa Chadema.
Hivyo alisema CCM isiogope kuangushwa katika uchaguzi huo kwani tayari wananchi wamejiandaa kutoa hukumu dhidi ya ugumu wa maisha kwa CCM na kuwa.
Hukumu ya madiwani wa Arusha Mbowe amepongeza hatua ya kushindwa kwa madiwani hao wa Arusha katika kesi hiyo na kuwa Chadema itaendelea kuwawajibisha madiwani na wabunge kigeu geu wanaotumiwa na CCM kutaka kuvuruga Chadema.
No comments:
Post a Comment