Wakazi wawili Mwanyanje kata ya Igawilo jijini Mbeya Bwana SEMENI MSAFIRI na Bwana LEVO MWANGALA wapo katika wakati mgumu baada ya nyumba yao kupigwa mawe yaajabu na watu wasioonekana.
Tukio hilo limekuwa likitokea majira ya saa kumi na mbili jioni hadi saa 4 usiku na kuanza tena saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa moja na nusu asubuhi.
Hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa mtaa wa Mwanyanje ELIA JEREMA (OBAMA) na amesema tukio hilo limedumu kwa muda wa mwenzi mmoja hadi sasa ambapo alipata taarifa kutoka kwa balozi wa mtaa huo Bwana PETER MWANIBUNGU ambapo kwa pamoja walimwita Chifu mdogo Bwana EDSON MWANYANJE ambaye pia alishindwa kutatua tatizo hilo na kudai kuwa kuna mapepo.
Lakini kwa siku ya jana aliitwa Chifu wa Mkoa Bwana MWASHINGA kutoka eneo la Spweto jijini Mbeya akiwa na machifu wengine na kutfanya kikao eneo la tukio na ndipo hali ikawa mbaya sana na hivyo kusababisha machifu kusambaratika na kutoa tamko kwamba hali ni ngumu baada ya kuanza kupigwa kwa mawe hayo na hivyo waende wakajipange upya hata hivyo mwandishi wa habari hizi aliamua kuvaa elemet/kofia ya pikipiki kujikinga ili kuendelea kupata habari hizi.
" Nimeshuhudia matukio mbalimbali katika nyumba ya Bwana SEMENI.yakionekana eneo hilo ikiwemo samaki wakavu aina ya magege wakipita angani, vikombe na sahani za udongo zikidondoka sakafuni bila kuvunjika, mafuta ya kupakaa aina ya Carorite, vikombe vya plastiki vitatu, hotpot moja, na mambo mengine yakiambatana na mawe, kama betri na mawe yaliyotengenezwa kwa saruji ambayo bado yalikuwa hayaonekani ambayo yalipelekea kuitwa Jeshi la Polisi Kituo kidogo cha Uyole ambapo walifika eneo hilo majira saa moja na dakika 45"
Picha za tukio zima tunazo endelea kutembelea mtandao huu.

No comments:
Post a Comment