Baadhi ya madereva waliogoma hapo jana wakishinikiza Serikali kutoa Tochi zinazotumika kuzuia mwendokasi barabarani, ili kuwapa fursa ya kusafiri kwa mwendokasi suala ambalo Mkuu wa Usalama wa barabarani Ezekiel Mgeni aligoma kuruhusu ombi hilo, na hayuko tayari kuvunja sheria kwani ajali nyingi za sababishwa na mwendokasi.
Mabasi yakitoka baada ya kusitisha mgomo kufuatia kauli ya Mkuu huyo wa Usalama wa barabarani ambapo aliwataka madereva ambao hawako tayari kufuata sheria za usalama wa barabarani warudishe Leseni na kwamba hayupo tayari kuona maisha ya watu wakiangamia na wengine kuwa walemavu.
Basi la Mbeya Express liliondoka stendi kuu baada ya kauli ya Mkuu wa usalama barabarani mkoani hapa.
Mwenyekiti wa Stendi kuu ya mkoa wa Mbeya Bwana Noah Mwakatumbula awaonya madereva watakao kaidi sheria za usalama wa barabarani watapambana na mkono wa sheria na hauyo tayari kuwatetea.
No comments:
Post a Comment