SAKATA la madiwani kutishia kumshushia kipigo Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo na Mwenyeykiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Erick Ambakisye limechukua sula mpya, baada ya Chama cha Mapinduzi wilayani humo kumwandikia barua diwani wake ya kumtaka ajieleze kutokana na kitendo alichokofanya kwenye kikao cha kutoa vitisho.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa barua hiyo yenye Kumb .Na. CCM/MBZ/VOL.1/112 ya Septemba 9 mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mwenezi wilayani hapa Clemence Mnkondya kwa imedai kuwa diwani kata ya Nkangamo Weston Simwelu alitoa kashifa kwa chama chake na kwa viongozi wa serikali ya wilaya ya Mbozi.
“Ulitoa maneno ya kashifa kwa chama chako cha mapinduzi na uongozi wake na uongozi wa serikali ya wilaya ya Mbozi pale uliposema; chukueni kikadi chenu cha chama cha mapinduzi sasa hivi, viongozi wa chama cha mapinduzi wa wilaya wote ni wanafiki na wajinga na mkuu wa wilaya ni mjinga na mpumbavu”ilisema sehemu ya barua hiyo.
Aidha kutokana na kukiuka kanuni za viongozi wa CCM ibara1.8 kabla hajachukuliwa hatua kali za kinidhamu kutokana na kashifa alizotoa kwa chama chake, viongozi na serikali yake ya wilaya anatakiwa ajieleze ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya barua hiyo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Diwani huyo Weston Simwelu amekana kupokea barua hiyo, lakini hata hivyo amedai kuwa juzi alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu akimwarifu aende achuke barua yake, hivyo anadhani huenda ikawa ndiyo hiyo.
Simwelu alipoulizwa juu ya kutakiwa kujieleza alisema kuwa kwa mujibu wa kanuni za baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya diwani anapofanya jambo lolote katika kikao cha baraza haruhusiwi kuhojiwa na chombo chochote.
Hata hivyo Diwani huyo alisema iwapo akipata barua hiyo atakuwa tayari kuijibu kwa mujibu wa kanuni husika ambazo alidai haziruhusu kuhojiwa.
Dalili za kutokuwapo amani katika vikao vya madiwani zilianza kuibuka Septemba 5mwaka huu katika kikao cha Kamati ya Mipango, Ujenzi na Mazingira diwani huyo alifanya fujo katika kikao hicho baada ya kutoelewana kwa hoja ya eneo la kuweka makao makuu ya wilaya mpya ya Momba na kusababisha polisi kuingilia kati kwa kuwashikilia madiwani wawili kwa muda
Ilipofika Septemba 7, mwaka huu wakati wa kikao maalumu cha baraza la madiwani wakijadili eneo la kuweka makao makuu diwani huyo alionesha utovu wa nidhamu kwa kumpinga wazi wazi mkuu wa wilaya hii Gabriel Kimolo kutokana na kitendo chake cha kusoma barua ya chama chake ikiwa ni msimamo wa chama hicho kuhusiana na ajenda iliyokuwa ikijadiliwa.
No comments:
Post a Comment